Aubameyang Ruksa Kurudi Arsenal

Kocha mkuu  wa timu ya taifa ya Gabon amemruhuhu mshamuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka kwenye michuano ya AFCON na kurudi klabuni kwake ili aende akajiuguze baada ya kupata maambukizi ya Uviko-19.

Vyombo mbali mbali vimeripoti kuwa alipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya moyo, lakini kocha wa timu hiyo hakuweza kuzungumzia swala hilo na kusema kuwa ulikuwa uamuzi sahihi tu wakuwarusu Aubameyang na Lemina.

Aubameyang

Kocha Patrice Neveu pia amemruhusu kiungo anayecheza Ufaransa Mario Lemina ambaye naye aliruhusiwa kurudi kwenye timu yake ya Nice amapo hakuweza kucheza hata dakika moja kwenye michuano hiyo, Aubameyang ni mchezaji wa pili kupewa ruhusa na kocha huyo.

“Tumefanya maamuzi sahihi kuwarudishwa  kwenye klabu zao wanaweza kuangaliwa vizuri wakiwa kule.” kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gabon Patrice Neveu

Gabon mpaka sasa kwenye michuano ya AFCON wamecheza michezo miwili kwenye kundi lao, huku wakiwa wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Comoro na wakiwa wametoka sare  na timu ya taifa ya Ghana, kwenye kundi wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi nne.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe