Hashtag ya #Agnelliout imeshika kasi kwenye mtandao wa Twitter ikiwa ni shinikizo la kumtaka raisi wa Juventus Agnelli kujiuzulu klabuni hapo, lakini klabu bado inasisitiza kuwa ataendelea kuwepo.

Bwana huyu, akiwa mmoja wa makamu wawili wa raisi wa Super League, na miungoni mwa watu muhimu zaidi kwenye mradi wa Super League ambaye alikiri kuwa mradi huo ni mgumu kuendelea baada ya timu sita za Premier League kujiondoa.

Kwa mujibu wa Spormediaset, Adrea Agnelli tayari ameshajitengenezea maadui wengi, na anaweza kujiuzulu kama raisi wa Juventus na nafasi yake kuchukuliwa na Alessandro Nasi.

Andrea Agnelli

Shinikizo la kujiuzulu kwa Agnelli linaendelea mtandaoni, mashabiki kibao wa soka, sio wa Juventus pekee, wote wakiwa wanasisitiza kuwa aachie kazi kama raisi baada ya sakata la Super League ambalo limeshika sura tofauti kwa mda mfupi mno vilabu vikubwa sita vikijiondoa.

Ed Woodward tayari ameshaweka wazi kuondoka United mwisho wa msimu na kuachana na kibarua chake kama makamu mwenyekiti. Kadri hali inavyoendelea, inawezekana raisi wa juventus anaweza kujikuta akiamua kuunga tela la kuachia ngazi.


 

MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Agnelli, Agnelli Ashikiwa Bango Aondoke!, Meridianbet

CHEZA HAPA

 

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa