Tangu atue Uingereza mwaka 2011 kutoka Atletico Madrid, Muargentina huyo jwa sasa amekuwa na historia kubwa sana ambayo sio suala dogo kuifikia hasa kwa umri wake wa miaka 30 hadi sasa. Na bado anatumainiwa kufanya makubwa zaidi ya hapo alipofika sasa na umaarufu anaoendelea kujikusanyia ndani ya taifa hilo la Uingereza.

Kwa sasa anaingia katika rekodi ya wachezaji waliozifungia klabu zao idadi kubwa ya magoli, ambayo ni zaidi ya 150. Katika rekodi hiyo Lampard pekee ameweza kufikisha idadi ya magoli 177 ndani ya taifa hilo. Kufuatia historia aliyoiweka baada ya kuwafunga Arsenal goli tatu na kuandika historia nyingine ya kufunga goli tatu ndani ya mechi ile. Baadhi ya wachezaji wanaoungana na Kun ni;

Wayne Rooney

Ameacha historia kubwa ndani ya taifa la Uingereza na kikosi cha Manchester United baada ya kufikisha magoli 208 ambayo ni hatua kubwa na yenye heshima kwa mchezaji wa aina yoyote. Kwa sasa anamalizia safari yake ya soka katika taifa la Marekani hususani katika klabu ya DC United ambako bado safari yake kufunga haijakoma. Ana historia ya kufunga magoli matatu ndani ya mechi moja [hat-triki] nane.

Robbie Fowler

Mashabiki wengi wa Liverpool hawatokuja kusahau jina na heshima aliyowawekea mchezaji huyo ndani ya klabu yao. Aliweka historia ya kufunga magoli 163 ndani ya ligi hiyo huku akiwa amefunga magoli matatu ndani mechi moja mara tisa. Mbali na hilo mchezaji huyo aliweza kuwafanya mashabiki wa Liverpool miaka ile waweze kupenda soka na ndio waliojenga heshima kubwa ndani ya kikosi hicho.

Andrew Cole

Maisha yake ndani ya klabu ya Newcastle yalikuwa yenye hatua kubwa baada ya kufunga magoli 34 ndani ya mechi 40 alizoichezea klabu hiyo. Mbali na hilo, aliweza kujiunga na Manchester United na kuendeleza historia chini ya Ferguson ambapo aliaminiwa na kuendana na falsafa ya mwalimu wake. Katika nafsi hiyo anaungana na watu kama  Alan Shearer, Jermain Defoe, Dimitar Berbatov na Agüero; wenye historia inayofanana na hiyo.

Thierry Henry

Hakuna mwenye kuweza kubisha juu ya uwezo wa mchezaji huyu katika enzi zake. Inakumbukwa 2004 aliweza kutajwa kama mchezaji bora wa Ulaya kutokana na nafasi yake na makubwa aliyoyafanya na klabu ya Arsenal miaka ya nyuma. Anaheshimika na kushukuriwa siku zote na klabu hiyo baada ya kuirudisha kwenye ramani zaidi klabu hiyo na kuipa vikombe. Aliweza kufunga magoli 175.

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa