Mfungaji wa muda wote wa timu ya Manchester City, Kun Aguero kuenziwa katika klabu hiyo kwa sanamu. Aguero ambaye amehudumu City kwa misimu kumi mfulululizo anategemewa kutimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utakwisha.

Aguero alitamani kuendelea kusalia klabuni hapo lakini alifanikiwa kuanza kwenye michezo mitano tu msimu mzima kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya goti toka Juni mwaka jana.

Aguero atakumbukwa kwa kuwa mfungaji bora wa Manchester City akiwa na jumla ya magoli 257 katika michezo 384 aliyocheza. Mfungaji huyu alivunja rekodi ya mfungaji wa muda wote wa city Eric Brooks toka mwaka 2017.

“Misimu kumi nikiwa nimepata mataji makubwa, na kipindi chote nilifanikiwa kuwa mfungaji wa kihistoria wa timu, na kutengeneza uhusiano mzuri na wanaopenda klabu hii – watu ambao watabaki milele moyoni mwangu” Alisema Aguero katika kurasa zake za kijamii.

Wakati Aguero akipokea habari za kuachwa kwa masikitiko, Mwenyekiti wa Manchester City Khaldoom Al Mubarak amethibitisha kwamba atawekewa sanamu la kumuenzi nguli huyo wa soka kutokea taifa la Argentina.

Kuondoka kwa Aguero kutawalazimu viongozi hao wa ligi kuu ya Uingereza kutafuta mfungaji, na straika wa Borussia Dortmund Erling Haaland anaweza kuwa shabaha sahihi.

Je, ni wapi Aguero ataenda baada ya City? Tupe maono yako!!

 


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

aguero, Aguero kukumbukwa kwa sanamu Etihad, Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa