Al Ahly leo watakuwa nyumbani Cairo International Stadium kucheza dhidi ya Simba katika mechi ya mwisho ya Kundi A, Ligi ya Mabingwa Afrika huku timu zote zikiwa zimefuzu tayari kwa hatua ya robo fainali.

Simba wataingia na kumbukumbu ya kuifunga Al Ahly goli 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, goli la Luis Miquissone.

Simba
Luis Miquissone

AS Vita na Al-Merreikh watacheza mchezo wa kukamilisha ratiba baada ya timu hizo kushindwa kufuzu kwa hatua inayofuata.

Simba
Gomes

Kuelekea mechi ya leo Kocha Mkuu wa Simba, Gomes amesema: “Tuna mchezo mgumu wa kucheza, mchezo muhimu kwetu kuwaonyesha kuwa tumekuwa timu kubwa na kwa uhakika tutamaliza kwenye nafasi ya kwanza kwenye hili kundi.”

“Hatuna majeruhi yeyote na tupo na kikosi kamili. Kesho tutaanza na kikosi chetu bora cha kwanza.”

Simba
Mosimane

Kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane amesema: “Kwa bahati mbaya tuna majeruhi kadhaa kikosini hivyo kuna mabadiliko ya lazima ambayo yanatulazimu kuyafanya na kwa hali ya mambo ilivyo wachezaji ambao huwa hawapati nafasi watalazimika kucheza, na ukiangalia mwezi mmoja uliopo mbele yetu una mambo mengi sana ambayo hatupaswi kufanya makosa kwa wachezaji wetu wengi zaidi kupata majeraha”

Simba ndio vinara wa Kundi A wakiwa na alama 13 mbele ya Al Ahly wenye alama 8 akifuatiwa na AS Vita yenye alama 4 na Al-Merreikh akiwa na pointi mbili baada ya kila timu kucheza mechi tano.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

simba, Al Ahly Vs Simba, Mechi ya Kisasi?, Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa