Kocha wa klabu ya Bayern Munich Nagelsmann amethibitisha kumuacha Alphonso Davies kutokana na matatizo ya moyo yaliogundulika baada ya kufanyiwa vipimo hivi karibuni.

Alphonso Davies amekosa mchezo wake wa kwanza mwaka 2022 ambao Bayern walishindi 2-1 dhidi ya Gladbach baada ya kukutwa na maambukizi ya Uviko-19, lakini kwa sasa amepima na kukutwa hana maambukizi na alitarajiwa kurudi mazoezi baada ya madaktari wa timu kuthibitisha.

Alphonso Davies
Alphonso Davies

Kwa bahati mbaya  kwenye vipimo kitu kisicho cha kawaida kikagundulika kwenye moyo na sasa atakuwa nje ya uwanja kwa muda akiendelea na matibabu ya moyo.

“Jana wakati tunafanya vipimo ambavyo tunafanya kwa kila mchezaji kujua kuwa ana maambukizi ya uviko-19, katikati ya kipimo tuligundua ishara isiyo ya kawaida kwenye moyo wa Davies, ila kwa sasa amesimama mazoezi, na hatakuwepo kwa wiki kadhaa zijazo.” Alisema Nagelsmann.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa