KLABU ya Yanga imefikia makubaliano ya kuachana na kiungo wa Kimataifa wa DR Congo Chiko Ushindi ambaye alikuwa anacheza kwa mkopo akitokea kwenye klabu ya TP Mazembe.
Chiko
Chiko
Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema kuwa uongozi kwa kushirikiana na bench la ufundi walifikia makubaliano ya mchezaji huyo kurejeshwa kwenye klabu yake baada ya kutumika kwa nusu msimu.

Manara alisema sababu kubwa ya  kumruhusu Chiko ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wakigeni kwenye timu hiyo lakini pia kufikia matakwa ya makubaliano baina ya Yanga na TP Mazembe.

Sambamba na hilo Manara alisema kwa upande wa winga wao Yakuba Sogne ataingia kambini pamoja na wenzake lakini yeye atakuja kukutana na uongozi ili kuzungumza naye katika kipindi hiki ambacho bado anahitaji kurejea kwenye ubora wake kabla ya kuanza kutumika.

Chiko
Chiko

Young Africans na Chiko Ushindi tumefikia makubaliano ya kumruhusu arejee kwenye klabu yake ya TP Mazembe kama ambavyo watu mnajua kuwa alikuwa anacheza hapa kwa mkopo.

“Yakuba yeye ataingia kambini na wenzake lakini atakutana na uongozi ili kujua namna gani watamsaidia kwa sababu ripoti yake ya mwisho ya madaktari ilionyesha kuwa bado hajakaa sawa.

“Hivyo viongozi wataangalia namna gani nzuri ya kumsaidia Yakuba kabla hajaanza kutumika au kwenda kutimika sehemu nyingine kabla hajapona vizuri na kuwa fiti,” alisema.

Manara pia aliweka bayana kuwa Yanga hawatasafiri kwenda nje ya Dar es salaam kwa ajili ya kambi na badala yake watabaki kambini kwao Avic Town na kambi hiyo itaanza rasmi Julai 21.


Kwa habari na Uchambuzi wa Kina kutoka meridianbetSport Unaweza kutazama video zetu 
Hapa 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa