Sababu kubwa na nzito iliyowafanya PSV wamsajili Ronaldo De Lima baada ya World Cup ya Marekani 1994, ni kasi yake.

Haaland, Erling Haaland kwenye Kivuli cha Ronaldo De Lima, Meridianbet
Ronaldo De Lima Akiwa PSV

Walijua mabeki Uholanzi na Ulaya nzima hawakuwahi kukutana na mshambuliaji wa kati mwenye kasi kama ya De Lima, hivo hawakuwa tayari kupambana nae. Walishawazoea mawinga wenye ‘mwendo wa duma’ lakini siyo washambuliaji wa kati.

Ushambuliaji wa Ronaldo kwao ulikuwa mpya kabisa. Mabeki walikiri kutokuwahi kumuona mshambuliaji wa kati mwenye shughuli kama yake. Msimu wa kwanza pale Uholanzi alirejea kambani mara 30.

Nimeweka picha ya Haaland hapo juu kwa makusudi halafu nikaanza na kisa cha De Lima kwa bahati mbaya. Huyu Halland alizaliwa mwaka 2000, De Lima akiwa staa pale Inter Milan. Nikuambie kitu kuhusu Halland?

Erling Haaland kwenye Kivuli cha Ronaldo De Lima

Huyu si Ronaldo de Lima, pengine hawafanani kabisa ila kisa chake cha usajili kinavutia. Nikusimulie kidogo?

Wakati kocha Lucien Favre anawasilisha ripoti yake kwa Mkuregenzi wa michezo wa Dortmund Hans-Joachim Watzke, kocha Lucien alimuambia Watzke, “Nataka kuunda timu ya mshambuliaji wa kujitegemea.”

Erling Haaland kwenye Kivuli cha Ronaldo De Lima

Wakati Watzke anataka kuuliza swali, kocha akamuambia, “Wala hili suala halihitaji maskauti, yupo mtoto wa miaka 19 atatufaa. Kumpata ni pauni 20 milioni tu. Yupo pale Salzburg. Huyo atatufaa.”

Erling Haaland kwenye Kivuli cha Ronaldo De Lima

Ndiyo huyu Halland anayetutishia akiwa Dortmund. Kocha wake Favre anadai, hii ni namba tisa mpya ambayo Ujerumani hawajawahi kuiona kabla. Hajui amfananishe na nani kiuchezaji.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Haaland, Erling Haaland kwenye Kivuli cha Ronaldo De Lima, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa