Infantino rais wa shirikisho la mpira duniani (FIFA) ameonesha kusikititishwa na kifo cha malkia Elizabeth kilichotokea jana huko Balmoral nchini Uingereza.

Malkia huyo ambaye anaingia kwenye vitabu vya historia kama mtawala alietawala kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya nchi hiyo kwa miongo saba ambaye atarithiwa na mwanae Prince Charles III ambaye atakua mfalme wa nchi hiyo.

infantinoMalkia anasifikia kwa kupenda michezo haswa mchezo unaopendwa zaodi nchini humo wa mpira wa miguu na tukio litakalokumbukwa zaidi ni pale alipompa tuzo ya Jules Rimet baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 1966 fainali zilizofanyika nchini humo.

Rais Infantino ametoa salamu zake za rambirambi na kusema kifo cha malkia ni pigo kubwa kwa jamii yetu ya mpira pamoja na ulimwengu wote na kwa upande wa jamii malkia alikua mkuu wa nchi kwa idadi ya vyama  vya wanachama wa FIFA na alikua mlezi wa soka kote Uingereza na mfuasi wa mchezo wetu kwenye jumuiya ya madola alisema Infantino.


Kwa ulimwengi na jumuiya ya kandanda Infantino amesema tumepoteza kiongozi wa kimataifa ambaye alishirikiana na kumtia moto kila aliyekutana naye,na kwa niaba ya soka duniani kote,mawazo yetu yako pamoja na familia ya kifalme katika wakati huu mgumu.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa