Chama cha Mpira wa Miguu Dodoma [DOREFA] kimetoa taarifa ya kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. Hamis Kisoyi kutokana na upotevu wa tiketi zenye thamani ya Tsh. 1,380,000 zilizopotea siku ya mchezo wa JKT Tanzania vs Yanga Mei 19, 2021.
Kaimu Katibu Mkuu wa DOREFA Bw. Hamsini amesema, Kamati ya Utendaji ilikaa ikapitisha kusikamishwa kwake ili taratibu nyingine zifuatwe.
“Sababu kubwa ya kusimamishwa kwa Katibu Mkuu ni upotevu wa tiketi, sasa yeye kama mtendaji mkuu wa chama inabidi awajibike ndio maana Kamati ya Utendaji imeanza kumsimamisha.”
Hamisi Kisoyi anasema bado taarifa za kusimamishwa bado hajazipokea lakini suala hilo [upotevu wa tiketi] tayari alishalifikisha kwenye vyombo vya usalama, anashangaa kusikia amesimamishwa kazi na kukuta ofisi aliyokuwa akiitumia imebadilishwa kufuli.
Hizi ndio changamoto zinazotokana na tiketi za ‘VISHINA’ kwenye baadhi ya viwanja.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.