’Leo Messi Stand’ Kuzinduliwa Kwenye Uwanja Mpya wa Imter Miami

Klabu ya Inter Miami CF imetangaza mpango wa kipekee wa kumuenzi nahodha wao Lionel Messi kwa kumpa jina la sehemu ya jukwaa katika uwanja wao mpya wa Nu Stadium. Hatua hiyo ni tofauti na ilivyozoeleka, kwani kwa kawaida heshima kama hiyo hutolewa kwa wachezaji waliostaafu.

’Leo Messi Stand’ Kuzinduliwa Kwenye Uwanja Mpya wa Imter MiamiKatika taarifa rasmi, klabu hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo unatokana na mchango mkubwa wa Messi kwa sasa, badala ya historia ya zamani. “Kwa kawaida, heshima kama hizi huangalia yaliyopita na kumbukumbu za zamani. Hii ni tofauti,” ilisema taarifa hiyo. “Hii imezaliwa kutokana na sasa—kile kinachotokea uwanjani na hisia unazopata kila mara Leo anapokanyaga dimbani.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Jukwaa hilo litajulikana kama ‘Leo Messi Stand’, likiwa sehemu ya uwanja mpya wa kisasa wa Nu Stadium wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 26,700. Inter Miami wanatarajiwa kucheza mchezo wao wa kwanza katika uwanja huo Aprili 4 dhidi ya Austin FC.

’Leo Messi Stand’ Kuzinduliwa Kwenye Uwanja Mpya wa Imter MiamiTangu ajiunge na Inter Miami mwaka 2023, Messi ameiongoza timu hiyo, inayomilikiwa kwa pamoja na gwiji wa zamani wa England David Beckham, kushinda mataji matatu makubwa. Mataji hayo ni pamoja na Leagues Cup mwaka 2023, MLS Supporters’ Shield mwaka 2024 na MLS Cup mwaka jana.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 pia ndiye kinara wa muda wote wa klabu hiyo kwa mabao na pasi za mabao, akiwa amefunga mabao 82 na kutoa asisti 53 katika michezo 94 aliyocheza. Hii inaonesha ushawishi wake mkubwa tangu ajiunge na klabu hiyo ya Marekani.

’Leo Messi Stand’ Kuzinduliwa Kwenye Uwanja Mpya wa Imter MiamiHivi karibuni, Messi alifikia rekodi ya kufunga mabao 900 katika maisha yake ya soka, na kuwa mchezaji wa pili kufanikisha hilo katika soka la wanaume baada ya mpinzani wake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.