Ligi Kuu ya Marekani, MLS, imethibitisha rasmi mpango wa msimu wa mpito wa mwaka 2027 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kubadili kalenda yake ili iendane na ligi nyingi za soka duniani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, msimu huo maalum utajulikana kama “MLS Sprint Season” na utaanza Februari hadi Mei 2027, ukiwahusisha timu zote 30 zitakazocheza jumla ya mechi 14 za msimu wa kawaida dhidi ya wapinzani wao wa ndani ya konferensi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mfumo huo mpya, kila timu itacheza na wapinzani wake wa conferens mara moja tu, iwe nyumbani au ugenini, katika kipindi cha Februari hadi Aprili. Timu nane bora kutoka kila conferens, Mashariki na Magharibi, zitafuzu hatua ya mtoano ya kuwania taji la MLS Cup, ambapo michezo yote itakuwa ya mtoano wa mechi moja moja hadi kufikia fainali itakayochezwa mwezi Mei 2027.
Mashindano hayo ya mpito pia yatatumika kuzipata timu zitakazoshiriki michuano ya kimataifa ya mwaka 2028, ikiwemo CONCACAF Champions Cup pamoja na Leagues Cup, ambayo hushirikisha klabu kutoka Marekani na Mexico.
Baada ya kumalizika kwa msimu huo wa mpito, MLS itaanza rasmi mfumo mpya wa msimu wa 2027/2028 utakaoanza Julai 2027 na kumalizika Mei 2028, huku fainali ya MLS Cup ikipangwa kuchezwa mwezi Mei 2028. Mfumo huu mpya utaifanya ligi hiyo kufuata kalenda inayotumika zaidi Ulaya na maeneo mengine duniani.
Katika msimu huo mpya wa 2027/2028, pia kutakuwa na mapumziko ya majira ya baridi katikati ya Desemba hadi mapema Februari, ambapo hakutakuwa na mechi zozote za ligi mwezi Januari. Wakati huo huo, msimu wa sasa wa 2026 unaoanza Februari hadi Desemba utafungwa rasmi kwa mchezo wa fainali ya MLS Cup utakaochezwa Desemba 18.


