Mastaa wengi duniani wameendelea kutoa pole kutokana na kifo cha Diego Maradona amefariki akiwa na umri wa miaka 60, siku za mwisho alifanyiwa upasuaji wa ubongo akiwa anaedelea vizuri na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Miongoni mwa mastaa ambao wametoa kauli kuhusu kifo cha Maradona ni pamoja na Lionel Messi raia wa Argentina ambaye alikuwa anatajwa kuwa mrithi wa Maradona na aliwahi kufundishwa na mkongwe huyo.

Maradona, Neno la Mwisho la Maradona kabla ya Kufariki, Meridianbet

Messi amesema kuwa ni siku ya kusikiitika kwa familia ya wanasoka wote duniani na Argentina inasikitika licha ya kuondoka bado anaishi.

Kifo kimemkuta akiwa nyumbani, mara baada ya kupata kifungua kinywa juzi, Novemba 25 Maradona inaelezwa kuwa alimuita mpwa wake, Johny Esposito na kutamka maneno mafupi,’ Me siento mal’ akimaanisha kuwa hajisikii vizuri kisha akarejea kitandani kulala.

Muuguzi wa kike ambaye alikuwa akisaidia kumuuguza baada ya kutoka hospitali baada ya kuona hivyo akapiga simu kuomba gari ya wagonjwa, ‘ambulance’ lakini hadi gari linafika nyumba aliyokuwa amepangisha alipokuwa akikaa baada ya kutoka hospitali Novemba 11 alikuwa amekata kauli.

Staa huyo wa zamani wa Napoli na Barcelona inaelezwa kuwa alipata shambulio la moyo na alikata kauli majira ya saa sita mchana kwa muda wa Argentina na taarifa zinaeleza kuwa taratibu za kuuaga mwili wa Maradona zitafanyika katika Ikulu ya Argentina.

Maradona, Neno la Mwisho la Maradona kabla ya Kufariki, Meridianbet


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

18 MAONI

  1. Familia ya mpira imepoteza mtu mahiri kupindukia uwanjani, inasemekana Pele alikuwa na uwezo huo tofauti yake ni kwamba alicheza wakati hakuna TV hivyo hatuwezi kuona uwezo wake kama Diego maradona

  2. Amecha pengo kubwa Sana wanasoka duniani kote wameumia Sana alikuwa mtu
    Muhimu ila kwa sasa amemaliza kazi yake tumwache apumzike kwa amani

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa