Baada ya ukimya wa muda mrefu, hatimaye bondia wa ngumi za kulipwa Amir Khan ameibuka na kudai yupo tayari kuvaana na muingereza mwenzake Kell Brook huko mjini manchester.

Amir Khan ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa anaamini kwamba sasa ni wakati sahihi wa yeye kupambana na Kell Brook. Bondia huyo wa Uingereza alipotea kwenye ulingo toka pambano lake la mwisho lililompa ushindi wa KO. Amir Khan alipigana na Billy Dib Julai 2019 na kumwangusha kwa KO, na kutoka hapo hakuonekana kwenye ulingo tena.

Amir Khan
Amir Khan katika moja ya mapambano yake

Akizungumza na Skysports, Amir Khan anadai kwamba amezungumza na promota wake Frank Warren kuhusu uwezekano wa kupambana na Brook huko Old Trafford.

Akiwa miongoni mwa mabondia bora duniani kuwahi kutokea, Khan anaamini bado yupo katika idadi ya mabondia 10 bora duniani na pambano lake la Brook litakuwa kubwa sana kutokana na wote kuwa waingereza.

Kinadaiwa kuwa kinachompa Khan kujiamini sana ni wakati mbaya alionao Brook toka apate jeraha la jicho wakati wa pambano lake mwaka 2016 dhidi ya Gennadiy Gollovkin.

Kulikuwa na taarifa zilizodai kuwa Khan alitaka kupambana na Floyd Mayweather ama Manny Pacquiao, lakini mambo yalishindikana kutoka na vikwazo vingi.

Bado timu ya Brook haijatoa jibu lolote kutokana na taarifa ya Khan. Je, Khan atafanikiwa kumshawishi Brook kupambana tena licha ya kupoteza katika mapambano yake makubwa toka 2017?


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Amir, Amir Khan Kupambana Na Kell Brook Old Trafford?, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa