Rais wa Barcelona Joan Laporta amethibitisha kuwa nyota Antoine Griezmann yupo sokoni kwenye dirisha hili la uhamisho wa msimu wa joto.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa akihusishwa na kurejea Atletico Madrid, huku vilabu kadhaa vya Ligi Kuu Uingereza vikitajwa kumfuatilia kwa ukaribu zaidi.

Laporta amesema kuwa mshambuliaji huyo ‘anapendwa’ na wababe hao wa Kikatalani, lakini shida za kifedha za klabu zinawalazimisha kumuweka sokoni mshindi huyo wa Kombe la Dunia.

Wakala wa Griezmann Awasiliana na Timu za EPL

“Griezmann ni mchezaji ambaye ana soko, na klabu zina nia, na tunaunda kikosi kinachofuata usawa wa kifedha,”

“Antoine, hatuna shida yoyote na yeye, tunampenda. Lakini ikiwa soko linapatikana, tuko wazi kwa kila ofa kwa sababu tuko katika wakati mgumu ambao tunapaswa kusawazisha usawa wa kifedha na kwa sababu hiyo, tunapaswa kuzungumza na wachezaji wote ili isiwaumize.

 
Joan Laporta

Mchezaji huyo wa miaka 30, ambaye amerudi kufanya mazoezi na Barcelona baada ya Euro 2020, amefunga mabao 35 na kusajili asisti 17 katika mechi 99 kwa timu yake ya sasa.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa