Arsenal wanatajwa kuwa hawatazamii kumrudisha Aaron Ramsey kwenye Uwanja wa Emirates kutokea Juventus msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales anaaminika kutaka kurudi kwenye Ligi ya Premia, miaka miwili baada ya kuondoka London Kaskazini kwenda Turin.

Ramsey hapo awali alikuwa na na Arsenal kwa misimu 11 kabla ya kuondoka kwa uhamisho wa bure, lakini wakati wake huko Juve haujaenda kama alivyotarajia.

Arsenal Kutemana na Mpango wa Kumrejesha Ramsey
Mfululizo wa changamoto ya majeraha umeathiri kampeni mbili za nyota huyu wa miaka 30, na Juventus inatajwa kuwa tayari kumuweka sokoni.

Arsenal ni moja ya timu zinazohusishwa na nyota wao wa zamani, lakini Goal inadai kuwa “hakuna nafasi” ya washika bunduki kutoa ofa.

Liverpool pia inaaminika ilionyesha nia kwa Ramsey, ambaye alifunga mabao mawili na kusaidia mengine manne katika mechi 22 za Serie A msimu uliopita.


 

SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa