Klabu ya Arsenal, inapanga kumuongeza mkataba mpya kiungo wake Granit Xhaka baada ya kuonekana itakuwa ngumu kupata mbadala wa mchezaji huyo katika majira haya ya kiangazi.

 

arsenal, Arsenal Wabadili Gia Angani kwa Granit Xhaka., Meridianbet

Kulingana na Jarida la The Athletic, Arsenal imebadilisha maamuzi yake juu ya kiungo huyo mswisi pamoja na kwamba klabu ya AS Roma ilikwisha peleka ofa kwaajili ya mchezaji huyo.

Xhaka alikuwa anatarajiwa kuachana na Gunners katika msimu huu wa joto baada ya kiwango chake kushuka katika msimu uliopita lakini kocha Mikel Arteta amebadili maamuzi baada ya kiwango alichokionyesha katika mashindano ya Euro 2020.

Xhaka bado ana mkataba wa miaka miwili na Arsenal, inasubiriwa kuona kama kiungo huyo atakubali kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo au atalazimisha kuondoka.


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa