Aston Villa wanaripotiwa kuwa tayari kukubali ombi la Manchester City la pauni milioni 100 kwa Jack Grealish.

Mabingwa wa Ligi Kuu wanaaminika kuwasilisha ofa kubwa Ijumaa, huku wakifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Aston Villa juu ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

Kwa mujibu wa Sky Sports News, kikosi cha Dean Smith bado kina nia ya kumshikilia mchezaji huyo na wameweka mezani mkataba mpya ulioboreshwa zaidi wakiamini staa huyu atazingatia kusalia klabuni hapo.

Jack Grealish Akubaliana Masharti na City

Hata hivyo, ripoti zinadai kwamba Villa wako tayari kukubali ofa ya Man City ya pauni milioni 100, ikimaanisha kuwa itakuwa ni juu ya Grealish kuamua kama anataka kuhamia Manchester.

Mchezaji huyo wa miaka 25 alifunga mabao saba na kuchangia asisti 12 katika mechi 27 kwenye za Aston Villa kwa kampeni ya 2020-21, huku akiitoa mchango kwenye mechi tano za Euro 2020.

Bosi wa City, Pep Guardiola anadaiwa anatamani saini ya Grealish ipatikane kabla ya kikosi chake kuingia dimbani kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City hapo Agosti 7.


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa