Azam FC Yathibitisha Kuongeza Mkataba wa Florent Ibenge Hadi 2028

 Azam FC imeweka wazi mustakabali wa benchi lake la ufundi baada ya kuthibitisha kumuongezea mkataba kocha wake mkuu, Florent Ibenge, ambao sasa utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2028.

Azam FC Yathibitisha Kuongeza Mkataba wa Florent Ibenge Hadi 2028Uongozi wa Azam FC umethibitisha taarifa hiyo kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii, ukisisitiza kuwa kocha huyo ataendelea kusalia “nyumbani” Chamazi licha ya uvumi uliokuwepo wa kujiunga na timu ya taifa ya Mali.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Taarifa ya klabu imesema “Florent Ibenge ataendelea kuwa sehemu ya Azam FC hadi mwaka 2028 baada ya makubaliano mapya ya mkataba kati ya pande zote mbili.”

Azam FC Yathibitisha Kuongeza Mkataba wa Florent Ibenge Hadi 2028Awali, Ibenge alisaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi, lakini mafanikio yake yameifanya klabu kumlinda kwa mkataba wa muda mrefu zaidi kutokana na mchango wake mkubwa.

Azam FC Yathibitisha Kuongeza Mkataba wa Florent Ibenge Hadi 2028Chini ya uongozi wake, Azam FC imefanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ya CAF Confederation Cup kwa kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza, huku pia ikiwa nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya NBC na pointi 52 ikibakiza mechi tano, sambamba na kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.