UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa utakuwa tofauti msimu huu kwenye kusaka ushindi wa mechi zote watakazocheza msimu mpya wa 2022/23.

Ofisa Habari wa Azam FC,Zakaria Thabit amesema kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo watacheza ili kupata pointi muhimu.

Azam

Jana Azam FC ilitarajiwa kutupa kete yake ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar,uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

“Tunataka mambo yawe kitofauti sana msimu huu hasa ukizingatia kwamba tumefanya maandalizi mazuri na mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco United imeweza kutupa nguvu.

“Abdul Suleiman,’Sopu’ aliumia mazoezini siku moja baada ya kurudi Misri ambapo tulikuwa tumeweka kambi pamoja na Idd Suleiman, ‘Nado’ ambaye alikuwa na maumivu kidogo kwa asilimia kubwa amepona ni suala la muda kuweza kurudi uwanjani.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa