Je ni Kweli Feitoto Amekuwa na Msimu Mzuri?

Zanzibar Finest Feisali Salum Abdallah Feitoto, nimekuita majina yako yote matatu, hongera sana kwa kiwango bora tangu ujiunge na klabu yako mpya ya Azam FC ukitokea kwa mabingwa mara 30 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga SC. Ilikuwa ni safari yenye hekaheka nyingi na vikwazo vilikuwa vingi sana lakini ushindi ukawa upande wako. Ushindi wa Meridianbet pia huedna ukawa kwako wewe mpenzi wa michezo ya kubashiri, Cheza hapa.

 

Feitoto

 

Uliwahi kusema kipindi uko Yanga ulikuwa unakula Ugali na Sukari ndiyo sababu ya kwenda kwa wana Rambaramba wa Chamanzi Azam FC, na kuwa na kiwango bora sana kuwahi kutokea kwenye maisha yako yote ya Soka.

Lakini je swali la kujiuliza ni kweli Feitoto amekuwa na msimu mzuri? Je msimu mzuri kwa mchezaji unapimwa kwa magoli ya kufunga?

Watu wengi wanamsifu sana Feitoto kwamba amekuwa na msimu mzuri sana kwa kufunga mabao 19 ambayo hayamfanyi kuwa mfungaji bora wa Ligi, Je nafasi ya pili kwake ni mafanikio?

Klabu yake ya Azam FC haijachukua ubingwa wa Ligi kuu, hivyo hana medali ya ubingwa wa Ligi je kwake kukosa medali ya ubingwa ni mafanikio?

Msimu wa 2021/22 akiwa bado yupo Yanga SC, Feitoto alishinda mataji yote muhimu ya ndani, alishinda ngao ya jamii, ligi kuu, na FA hapa sasa unaweza kusema alikuwa na msimu mzuri.

Lakini kwa mafanikio binafsi ya mchezaji, Feitoto anaingia kwenye kundi la wachezaji wachache wa Ligi Kuu wenye mafanikio pekee/ binafsi kwa kuisaidia timu yake ya Azam FC kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika, hii ni baada ya kuhangaika kwa takribani misimu 10.

Amefunga jumla ya mabao 19 kitu ambacho sio cha kawaida kwakwe tangu aanze kucheza soka la kulipwa, ni moja ya viungo washambuliaji wachache wazawa kuwa na namba hizo, huku John Raphael Bocco ndiye akiwa kinara wa ufungaji kwa wachezaji wazawa kwa miaka ya hivi karibuni kufikisha mabao angalau 20 kwa msimu mmoja.

Meridianbet ni chimbo zuri la kutengeneza pesa, hakikisha unajiunga na familia ya mabingwa ili uwe moja ya washindi wengi. Cheza kasino ya mtandaoni pia kwa ushindi wa Mamilioni.

Acha ujumbe