Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imetangaza rasmi kumsajili kiungo mkabaji wa kimataifa wa Tanzania, Adolf Bitegeko, kutoka Azam FC ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kikosi kuelekea msimu mpya.
Bitegeko mwenye umri wa amejiunga na Kaizer Chiefs kwa ada ambayo haijawekwa wazi. Kabla ya kujiunga na Azam FC mwezi Januari 2024, kiungo huyo aliwahi kuzichezea klabu kadhaa nchini Iceland na pia alikuwa nahodha wa Azam FC.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kupitia taarifa rasmi, Kaizer Chiefs imesema usajili wa Bitegeko umeandika historia kwani ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kuichezea klabu hiyo maarufu inayojulikana kwa jina la Amakhosi.
“Kiungo mkabaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikuwa nahodha wa Azam FC, anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kujiunga na Amakhosi. Ujio wake unaongeza orodha ya wachezaji kutoka zaidi ya nchi 20 za Afrika waliowahi kuvaa jezi yetu ya dhahabu na nyeusi,” ilisema Kaizer Chiefs katika taarifa yake.
Bitegeko aliichezea Tanzania katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), huku akicheza mechi zake zote tano za kimataifa mwaka 2024. Kaizer Chiefs pia imewasajili beki Thabo Moloisane na kipa Renaldo Leaner kama sehemu ya kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.


