Kocha Msaidizi wa zamani wa vilabu vya Azam FC na Biashara United Bahati Vivier amelamba dili la kuwa kocha mkuu nchini Burundi kwenye timu ya Bumamuru itakayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

Timu hiyo inatarajia kushiriki ligi kuu ya Burundi kwa msimu unaoanza hivi karibuni ambapo tayari kocha huyo ameshaanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kwa ajiri ya mashindano yote ya msimu unaotarajia kuanza hivi karibuni.

azam, Kocha Azam Alamba Dili Burundi, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Vivier amesema kuwa “nimerejea Burundi muda mrefu
kabla hata ya kumalizika kwa ligi msimu uliopita nilivyokuwa na Biashara
United.

“Kwa sasa ninakinoa kikosi cha Bumamuru ni timu ya huku Burundi na
malengo yangu kwa sasa ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema kwenye
ligi.” 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa