Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema timu yake haina sababu ya kuficha mbinu zao kuelekea mchezo ujao dhidi ya Yanga SC, akisisitiza kuwa wapinzani wao tayari wanaifahamu vizuri Azam kutokana na mechi nyingi walizocheza msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Dodoma jiji fc na Kushida mabao 3-0 aliulizwa kuhusu uwepo wa wawakilishi wa wapinzani kwenye mchezo wake uliopita dhidi ya Dodoma Jiji FC, Ibenge alisema,“Ni jambo la kawaida. Kama ningekuwa katika hali hiyo pia ningekuja kuutazama mchezo wa mpinzani wangu.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo ameongeza kuwa Azam FC haina kitu cha kuficha kwa sababu mfumo wao wa uchezaji tayari umeonyeshwa wazi katika mechi kadhaa zilizopita, jambo linalowafanya wapinzani kuwa tayari kuelewa mbinu zao.

Hata hivyo Ibenge alisisitiza kuwa lengo la timu yake ni kuendelea kuimarisha utendaji uwanjani na kuhakikisha wanapata matokeo chanya, bila kuathiriwa na uwepo wa wawakilishi wa timu pinzani. Kwa sasa, Azam FC inajiandaa kwa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga, huku kocha akisisitiza umuhimu wa umoja na kuzingatia mbinu bora ili kufanikisha ushindi.

