Mayele Fiston Kalala amefunga magoli matatu kati ya manne waliyoshinda Yanga katika mchezo wa hatua ya awali wa klabu bingwa Afrika uliopigwa katika dimba la Benjamin William Mkapa.

Mchezo ambao klabu ya Yanga walikua ndo wageni dhidi ya klabu ya Zalan kutoka Sudan kusini ambao wameomba kutumia uwanja wa Mkapa kama uwanja wao wa nyumbani kutokana na sababu tofauti tofauti waliweza kukumbana na kipigo kizito kutoka timu timu ya wananchi katika uwanja huo.

mayeleKatika mchezo huo ambao Yanga walionekana kuutawala kwa kiwango kikubwa kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo mpaka dakika tisini zinatamatika mabingwa hao wa Sudani kusini waliweza kupambana mpaka kipindi cha kwanza kinakwishwa walikua bila bila.

Mapema kipindi cha pili si mwingine ni Fiston Kalala Mayele alienza kufungus ukurasa wa magoli kwa klabu ya Yanga kabla ya Feisal salum kuandiks bao la pili ndipo Mayele alipohitimisha Hatrick yake ya kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kufunga goli la tatu na la nne la mchezo huo.

Yanga wanajiweka katika mazingira mazuri kuelekea hatua nyinginge kufuatia ushindi huo mnono walioupata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa