POINTI moja waliyoipata Azam kwenye mechi dhidi ya Geita Gold baada ya kutoka sare ya bao 1-1 imemkera kocha Mkuu wa Azam, raia wa Somalia, Abdihamid Moallin.

Bao la Azam FC kwenye mchezo huo limefungwa na kinda, Tepsie Evance ’41’ huku bao la kusawazisha la Geita likifungwa na Adeyum Saleh ’54’.

Azam, Sare Yamkera Msomali Azam, Meridianbet

Akizungumzia matokeo hayo Moallin amesema kuwa: “Kipindi cha kwanza tulimiliki vizuri mchezo lakini kipindi cha pili tulishindwa kutawala mchezo kitu ambacho kiliwapa wapinzani wetu morali ya kusawazisha.

“Tuna kikosi kizuri, tuna matumaini makubwa hivyo tunahitaji kubadilika na kujifunza kwani ligi ni ngumu na kila mpinzani tunayekutana naye ni changamoto kwetu. 

“Sijafurahia matokeo ambayo tumeyapata kwenye uwanja wetu wa nyumbani ila tunaenda kwenye kiwanja cha mazoezi kwa ajili ya kulifanyia kazi ili kuhakikisha kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Yanga mapungufu hayo hayajitokezi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa