Singida Black Stars, Azam fc Kwenye Vita ya Kusaka Alama tatu

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa leo katika dimba la Airtel Stadium, Singida, kati ya Singida Black Stars na Azam FC, pande zote mbili zimeonyesha utayari mkubwa huku kila mmoja akilenga kuibuka na ushindi.

Singida Black Stars, Azam fc Kwenye Vita ya Kusaka Alama tatuKocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema wanafahamu ugumu wa mchezo huo lakini wamejiandaa kupambana kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu. “Tunajua itakuwa ngumu, lakini akili yetu ni kwenda uwanjani kupata ushindi,” alisema Ibenge akielezea dhamira ya timu yake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa 

Kwa upande wa wachezaji, kiungo wa Azam FC Nathaniel Chilambo ameweka wazi malengo yao, akisisitiza kuwa hawapo tayari kupoteza wala kuridhika na sare. “Kwa maandalizi tuliyonayo, tunahitaji ushindi tu,” alisema Chilambo.

Singida Black Stars, Azam fc Kwenye Vita ya Kusaka Alama tatuNaye Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Othmen Najjar, amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa kuzingatia mbinu za ushambuliaji na ulinzi ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. “Tumejipanga vizuri, kikubwa ni nidhamu, umakini na kujiamini,” alieleza Najjar.

Singida Black Stars, Azam fc Kwenye Vita ya Kusaka Alama tatuMchezaji wa Singida Black Stars, Ayoub Lyanga, amesema wanataka kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani. “Lengo letu ni kushinda mbele ya mashabiki wetu,” alisema Lyanga, akionyesha ari ya timu hiyo kuelekea pambano hilo muhimu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.