BAADA ya kusajiliwa Azam, straika, Abdul Sopu ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo kwa msimu ujao.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha kubwa kutokana na kiwango alichoonyesha akiwa na timu ya Coastal Union ya Tanga.

Azam, Sopu Mashabiki wa Azam Wasubiri Furaha, Meridianbet

Sopu alikuwa mchezaji nyota kwenye mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho, huku akifanikiwa kufunga goli tatu kwenye mchezo huo.

Akizungumzia hilo, Sopu amesema kuwa “Ni furaha kubwa kwake kujiunga na klabu hiyo na haukuwa uamuzi mgumu kwa upande wake.

“Kujiunga na Azam haikuwa ngumu kwangu kwani ni timu yangu ya nyumbani, ni furaha kubwa kwangu kuwa hapa nawaomba mashabiki watusapoti kwani tumepanga kuwapa furaha kwa msimu ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa