Mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Abdul Suleiman ‘Sopu’ ameonyesha kuwa na mzuka wa kuanza maisha yake mapya kwenye klabu ya Azam ambapo amefunguka kuwa mashabiki na viongozi timu hiyo wategemee makubwa kutoka kwake.

Sopu ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu na lamba lamba, amesema kuwa anatambua ukubwa wa timu hiyo lakini kwa kiasi fulani ana uzoefu wa kucheza kwenye timu kubwa kwani aliwahi kuitumikia Simba miaka ya nyuma.

Azam, Straika Azam aahidi jambo, Meridianbet

“Presha kwa mchezaji ni jambo la kawaida na muda mwingine huwa chachu kwa mchezaji kufanya vizuri, hata Coastal kuna muda wachezaji tulikuwa tukikumbana na presha kwa sababu timu ilikuwa ikihitaji kumaliza msimu vizuri.

“Natambua Azam ni timu kubwa na nisingependa kuwa mzungumzaji sana, lakini ahadi yangu ni kutoa mchango wangu kwa asilimia 100, kama ilivyokuwa Coastal ili kufanikisha malengo ya timu na kuwafurahisha mashabiki.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa