Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wameripotiwa kuelekeza nguvu zao kwa winga wa Azam FC, Idd Seleman ‘Nado’, katika jitihada za kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa mashindano.
Hatua hiyo inakuja wakati mkataba wa Nado na Azam FC ukielekea kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu, huku taarifa zikidai kuwa pande zote mbili bado hazijafikia mwafaka wa kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kushirikiana.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Yanga wameonyesha nia ya kumsajili Idd Nado kutokana na uzoefu wake na uwezo wake mkubwa wa kucheza katika nafasi za pembeni za ushambuliaji,” zimeeleza taarifa zinazohusiana na harakati za usajili wa klabu hiyo.
Inaelezwa kuwa nyota huyo amependekezwa ndani ya Yanga kama mchezaji atakayesaidia kuziba pengo la mawinga wazawa, huku akionekana kuwa na sifa zinazohitajika kuendana na malengo ya timu hiyo ya kutetea mataji yake ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.
“Harakati za Yanga kwa Nado ni mwendelezo wa ushindani wa usajili kati yao na Azam FC, ambao hivi karibuni pia walikabiliana katika mbio za kuwania saini ya Henock Molia wa FC Lupopo.” Nado amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Azam FC msimu huu baada ya kucheza mechi 19 kati ya 25 na kufunga mabao manane.


