Wanalalamba wa Chamazi, Timu ya Azam FC imefanikiwa kujikita kwenye mbio za kuwania ubingwa wa VPL sawa na vinara Simba na Yanga, baada ya hapo jana kuibuka na ushindi mnono wa 2-0 dhidi ya biashara United.

Ushindi huo wa jana wa Azam FC, umefanya timu hii kurudisha matumaini ya kuwania kombe la VPL, na kurudisha matumaini ambayo yalionekana yakififia hapo awali.

Magoli ya Prince Dube ambaye amefikisha magoli 14 mpaka sasa, huku akiwa kinara wa wafungaji wa VPL, na lile la shujaa asiyeimbwa Mudathir Yahya yaliwafanya wanalambalamba hawa matajiri wa Dar es salaam, kufunga biashara kwa ushindi muhimu.

Alama tatu walizopata jana Azam zinawapeleka mpka nafasi ya tatu na wakishika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Yanga kwa alama moja na michezo kadhaa.

Azam

Vita ya VPL itasalia kwa timu hizi tatu za juu kwani kwa michezo iliyobaki hakuna timu yeyote inayoshika nafasi ya nne na kuendelea itaweza kurudi kufikisha alama 60 zilizokuwa kwa Azam ambayo inashika nafasi ya tatu.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa