Prince Dube, Mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC jana alikuwa nyota wa mchezo wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam 2-0 Mtibwa Sugar kwa kutupia mabao yote mawili.

Azam
Prince Dube

Dakika ya 8 alipachika bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Mudathir Yahya ambaye alichezewa faulo ndani ya 18 na lile la pili alifunga dakika ya 86 na kuifanya Azam kusepa na pointi tatu mazima.

Ushindi huo unaishusha Simba nafasi ya pili mpaka ya tatu kwa kuwa Azam FC imefikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 25 na Simba ina pointi 46 ikiwa imecheza mechi 20 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 50.

Azam

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-0 Azam hivyo jana kisasi kimelipwa. Dube anafikisha jumla ya mabao 10 akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

azam, Azam Yaishusha Simba Nafasi ya Pili, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa