Nahodha wa Chelsea – Cesar Azpilicueta, amkingia kifua golikipa wa timu yao – Keba Arrizabalaga baada ya kuandamwa na wapenzi wa soka.

Kepa amekuwa kwenye kiwango cha chini kwa muda sasa licha ya kuendelea kuaminiwa na kocha Frank Lampard. Mitandao ya kijamii na baadhi ya wachambuzi wa soka wamekuwa akimsema sana kwa kiwango duni.

Kushuka kwa kiwango cha Kepa, kulimfanya Lampard aingie sokoni na kumsajili Edouard Mendy. Pamoja na usajili huo, bado nafasi ya Kepa kwenye kikosi cha Chelsea ipo. Azpilicueta anaamini Kepa atarejea katika ubora wake bila shaka yoyote.

“Kwenye maisha ya soka, tunapitia nyakati ngumu. Kwa nafasi yangu kama nahodha, Kepa ninamfahamu kwa muda mrefu sana, kila mara ninajaribu kumsaidia.

“Ni kweli kunaugumu na muda mwingine unahisi kama kila kitu kinapingana na wewe. Unahitaji kuwa na uwezo wa kupambana na hilo na kufanya bidii. Sina shaka, Kepa atafanya kila awezalo ili kurejea kwenye ubora wake.

“Timu nzima tunalengo moja na tunapambana kwa umoja wetu kufikia lengo, kila mmoja anahitajika. ”

Azpilicueta anaiongoza Chelsea ambayo inashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na pointi 8 katika michezo 5 waliyoicheza. Chelsea wataitupa karata yao ya kwanza kwenye mashindano ya UEFA jumatano hii dhidi ya Sevilla.


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

29 MAONI

  1. Vizuri kadri siku zinavyo enda anazidi kukaa sawa kushuka kwakiwango nichangamoto ndogo ndogo ila bado anaitambua kaz yake Arrizabalaga

  2. Lawama yingi zinamuangukia kepa me nao a hitakua suruisho lake so kutakua na ushindani mkubwa kati ya yeye na goli kila mwenzake na mda pia wa kupunzika na kutumia akili hataupata ukiangalia kepa ameipambania sana Chelsea vya kutosha bado hana umuimu wake pale clabuni

  3. Kepa yupo vzr kocha lampard hawez tena kumuamin kutokana na kufungwa magoli ya kizembe ila kepa yupo vzr ukizungumziah magoli kipa bora huwez kumkosa kepa hv now

  4. Vizuri kadri siku zinavyo enda anazidi kukaa sawa kushuka kwakiwango nichangamoto ndogo ndogo ila bado anaitambua kaz yake Arrizabalaga

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa