Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Abdi Kassim Sadallah (Babi) baada ya kustaafu kucheza Soka kwa sasa amejikita kwenye ukocha na anatambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) baada ya hivi karibuni kumaliza Mafunzo ya ukocha ngazi ya Diploma C .

Babi ambaye aliwahi kuwika kwenye vilabu vya Mlandege, Mtibwa Sugar, Yanga pamoja na Azam amesema timu yoyote ikihitaji huduma yake ya ukocha anazikaribisha kwani kwa sasa hiyo ndio kazi aliyoichagua.

“Mimi ukocha sijaanza leo wala jana, nilipata uzoefu tangu nikiwa Yanga baadhi ya mechi licha yakuwa ni captain lakini pia wakati mwingine nasimama kama kocha, hii kazi naipenda ikija timu yoyote kutoka Pemba, Unguja, Bara au popote mimi nipo tayari najua kazi hii inachangamoto lakini nitapambana nayo”.

Babi amezaliwa Oktoba 19, 1984 ambapo Watanzania wataendelea kumkubuka kwa kuandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa Taifa (Kwa sasa unaitwa uwanja wa Mkapa) wakati ukifunguliwa mwaka 2007 ambapo alifunga bao hilo akiwa umbali wa mita 35 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ambao uliopigwa Septemba Mosi, 2007 na Taifa Stars kushinda 1-0.

Mbali na rekodi hiyo, pia anakumbukwa na mashabiki wa Azam FC kwa rekodi yake ya kufunga bao la kwanza kwa timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Nasri ya Sudan uliopigwa Februari, 2013 kwenye Uwanja wa Taifa (Kwasasa Uwanja wa Mkapa).


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa