Kiungo na mchezaji wa klabu ya Manchester United, Ander Herrera anasema bado haelewi kama ataendelea kusalia klabuni hapo msimu ujao japo hajawahi kufikiria kabisa kuihama klabu hiyo lakini kwa hali inavyoendelea ameamua kukaa kwa tahadhari kwa kucheza nafasi mbili kwa wakati mmoja.

Baada ya kuona mkataba wake uko ukingoni na hakuna uelekeo wowote wa kuongeza mkataba kwa wakati huu ameamua kuwasiliana na wakala wake aweze kuendeleza mazungumzo na klabu yake hiyo huku akiendelea kuangalia klabu nyingine zinazoweza kuhitaji huduma yake kutokana na mambo kuwa njia panda juu ya baadaye yake.

Mkataba wa mchezaji huyo umefika ukomo wake kwa sasa na mapema mwezi wa sita atakuwa mchezaji huru kufanya lolote lililo bora kwake. Kiungo huyo mwenye miaka 29 amewatamanisha Wafaransa, PSG uwezo wake kwa kuona kwamba anaweza kuwa na msaada endapo atatua kwenye kikosi chao.

Kwake kama mchezaji jambo kama hili sio la kustaajabisha. Anaona kwamba fununu ni jambo la kawaida sana kutokana na wakati uliosalia kwenye mkataba wake. Amebakiza miezi mitatu ndani ya mkataba wake; hivyo masuala kama hayo ya fununu hayawezi kuzuilika kwa kipindi hiki ila kila kitu kitatulia tu mahali pake kwa wakati.

Bado Upepo Hausomeki…

Na amekiri kwamba kila kitu amekiacha chini ya mikono ya wakala wake; iwe ni katika kuweka vizuri suala zima la yeye kuongeza mkataba kikosini hapo au iwe nje ya klabu hiyo kwa sasa. Japo akili yake yote kwa sasa ipo kuendelea kusalia hapo kwani ni klabu ya ndoto yake kwa miaka mingi na ana furaha kuwepo hapo.

Herrera amekuwa akifanya mazungumzo ili kujihami kama klabu yake ya United itaweka mazingira ya kutemana naye maana hajapata wakati wa kucheza muda mrefu nje ya klabu hiyo. Amekaa klabuni hapo kwa kipindi kirefu na kujiwekea mazingira ya mashabiki kuelewa mchango wake ndani ya klabu hiyo.

Furaha yake klabuni hapo ni upendo anaooneshwa na mashabiki wa klabu hiyo. Kutokana na kumjali walikoonesha, kumpa nafasi ya kuichezea klabu yao hiyo kwa kipindi chote hicho; na kikubwa kinachompa furaha kikosini hapo ni uwepo wa mashabiki hao ambao hujitokeza kuisindikiza timu yao wakati wowote na yeye anapendezwa kulipa fadhila kwa hilo.

Kama United watamuachia mchezaji huyo kiuhalisia watakuwa wamefanya kosa kubwa sana kwa wakati huu. Sio wakati sahihi kumuachia mchezaji ambaye ubora wake hauchuji hata akikaa muda mrefu bila kucheza uwanjani. Hivyo, kwa wakati huu hawapaswi kufanya kosa kama hilo maana linaweza kuwagharimu na wakajutia maamuzi yao.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa