Luis Miquissone, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba amesema kuwa kwenye mabao yake matatu ambayo amefunga ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika lile alilowatungua Al Ahly kwake ni moja ya bao bora kwa sasa.

Bao la kwanza Luis alifunga mbele ya Al Ahly wakati Simba ikishinda bao 1-0, bao la pili aliwatungua Al Merrikh, wakati Simba ikishinda mabao 3-0 na bao la tatu aliwatunga AS Vita, wakati ubao ukisoma Simba 4-1 AS Vita na yote alifunga Uwanja wa Mkapa.

Luis
Luis Miquissone dhidi ya Al Merreikh

Luis Miquissone ambaye ni miongoni mwa nyota waliokwea pipa leo kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili 9 amesema kuwa furaha yake ipo kwenye ushindi wa timu yake.

“Ninapenda kuona timu ikishinda na bao langu bora kwa sasa ni lile nililofunga dhidi ya Al Ahly,“.

Bao hilo la Luis lilichaguliwa kuwa bao bora la wiki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika, (CAF).


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa