Miamba wa Uhispania Barcelona wameripotiwa kujiondoa kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway ni mmoja wa wanasoka wanaotafutwa sana huko Uropa na amekuwa akihusishwa sana na kuhamia Barcelona, pia Manchester City, Manchester United, Chelsea na Real Madrid.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Uhispania TV3, Barcleona atahitaji kutoa karibu milioni 150 ikiwa wanataka kumsajili Haaland msimu huu wa joto na ikiwa ni pamoja na kuweka mezani ofa kubwa ya mkataba.

Barcelona Wajiondoa Mbio za Kumnasa Haaland

Barca kwa sasa wana deni zaidi ya zaidi ya Pauni 1 na hii ni kwa sababu ya shida yao ya kifedha, usajili wowote wa mchezaji huko Uropa, ikiwa ni pamoja na Haaland, utakuwa mgumu kutekelezeka.

Habari zaidi ni kuwa kipaumbele cha kilabu hiyo ni kuhakikisha kwamba Lionel Messi, ambaye anaweza kuondoka klabuni bure mwezi ujao anasaini mkataba mpya kusalia Camp Nou kwa zaidi ya kampeni hii.

Haaland, mwenye miaka 20, amecheza mechi 40 za mashindano akiwa na Dortmund hadi sasa msimu huu, akifunga mabao 39 na kutoa asisti 12.


 

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Barcelona, Barcelona Wajiondoa Mbio za Kumnasa Haaland, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa