Barcelona imeangukia kukutana Sevilla katika droo ya nusu fainali ya Copa del Rey ikiwa Ronald Koeman yupo kwenye kutafuta taji lake la kwanza tangu achukue jukumu la kuionoa timu hiyo ya LaLiga.

Barcelona Uso kwa Uso na Sevilla Katika Cop del Rey.

Timu hizo zinakutana tena wakiwa na kumbukumbu ya kukutana katika robo fainali ya michuano hiyo miaka miwili iliyopita, wakati Sevilla ilipoifunga Barcelona 2-0 kabla ya kwenda Camp Nou ambako walipokea kipigo cha 6-1 na kuondoshwa kwenye michuano.

Koeman ambaye alichukua mikoba mwezi Agosti tayari ameshuhudia timu yake ikifungwa 3-2 na Athletic Bilbao katika fainali Supercopa de Espana mwezi uliyopita na Messi alitolewa kwa kadi nyekundu wakati wa extra time.

Walikuwa karibu kutolewa katika robo fainali wiki hii na Granada, waliokolewa na mabao ya dakika za mwishoni katika muda wa kawaida kutoka kwa Antoine Griezmann na Jordi Alba kabla ya kushinda 5-3 baada ya muda wa nyongeza.

Kukabiliana na Sevilla hakika haitakuwa kazi rahisi kwa Barca, ya pili katika LaLiga, iko hatua tu mbele ya timu ya Julen Lopetegui.

Kunaweza kuwa na fainali nyingine kati ya Barcelona na Athletic , wakati miamba ya Bilbao wakipangwa kukabiliana na Levante katika nusu fainali nyingine.

Mechi ya mzunguko wa kwanza itachezwa katikati ya wiki ijayo, na michezo ya kurudiana itachezwa katikati mwa wiki ya kwanza mwezi Machi, na tarehe kamili za kila mechi kuamuliwa.

Sevilla watakuwa na motisha ya ziada kufikia fainali, ikizingatiwa kuwa mechi hiyo itafanyika katika jiji lao Aprili 17, huko Estadio La Cartuja.

Barcelona inashikilia rekodi ya kubeba mataji mengi zaidi ya Copa del Rey, ikiwa imeshinda mashindano hayo mara 30, na Athletic ilifuata kwenye orodha na ushindi 23.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa