Mambo mengi yamekuwa yakiendelea Barcelona, suala kubwa likiwa ni kuhusu kiwango cha klabu kipindi hiki, na mabadiliko kadhaa klabuni hapo.

Wakati suala la uhamisho wa Lionel Messi kuchukua sehemu kubwa ya vichwa vya habari vinavyohusu klabu ya Barcelona, mambo kadhaa yamekuwa yakiendelea Barcelona nyuma ya pazia, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya kiuongozi.

Wakiwa chini ya uongozi mpya wa raisi Joan Laporta, Barcelona wamethibitisha mapema wiki hii kuondoka kwa aliyekuwa mkurugenzi wa klabu Oscar Grau.

Kwa takribani kipindi cha wiki sita zilizopita, Barca wamekuwa wakifanyia kazi nafasi mbalimbali kwenye bodi, suala linaloshikiliwa na raisi Laporta. Ferran Reverter anatajwa kuwa mrithi wa Oscar Grau akiungana na watu muhimu wengine kwenye bodi ya wakurugenzi.

Joan Laporta Raisi Mpya Barcelona.
Joan Laporta

Barcelona wamethibitisha pia kuteuliwa kwa Xavi Budo kama mkurugenzi wa michezo ambaye katika majukumu yake anatarajiwa pia kusimamia mfumo wa kuendeleza vijana klabuni hapo, na kitengo cha soka la wanawake.

Xavi Budo alikuwa sehemu muhimu ya ushindi wa wa Laporta kama raisi mpya wa klabu hiyo, kwa mujibu wa Mundo Deportivo.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa