Huu ni msimu ambao pengine tutajionea mengi kunako ligi mbalimbali za soka barani Ulaya. Kwenye LaLiga, mambo yanaanza upya! Barcelona itakuaje sasa?

Mbio za ubingwa wa LaLiga zinaanza upya ikiwa imesalia michezo 5 msimu wa 2020/21 kumalizika. Barcelona wamepoteza nafasi ya kuwazidi wapinzani wao kwa pointi 2 baada ya kufungwa na Granada.

Hii ni mara ya kwanza kwenye histori ya Granada kuwafunga Barca katika dimba la Camp Nou. Lionel Messi alifanya kazi nzuri akishirikiana na Antoinne Griezmann kufunga goli la kwanza.

Barcelona, Barcelona Yatikiswa na Granada Camp Nou., Meridianbet
Jorge Molina akishangilia goli lililozamisha jahazi la Barca pale Camp Nou

Hakika siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Barca walishindwa kuzitumia nafasi nyingi za magoli walizozipata. Darwin Machis aliwapatia Granada goli la kusawazisha kabla ya Jorge Molina (akitokea benchi) kupigilia msumari wa moto kunako dakika ya 79 na mchezo kumalizika kwa matokeo ya 2-1.

Kufungwa kwa Barca kunawaeka kwenye nafasi ya 3 wakizidiwa pointi 1 na vinara wa LaLiga, Atletico Madrid huku wakiwa sawa na mahasimu wao Real Madrid.

Mei 8,2021 pengine mbivu na mbichi zitajulikana katika kuwania ubingwa wa LaLiga msimu huu. Barcelona watachuana na Atletico Madrid, ni Ronald Koeman au Diego Simeone atakayeibuka kidedea?


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa