Ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya mwekezaji wa Simba Mo Dewji kutoa maelezo yanayoonekana kuwa na hali ya masikitiko na kukata tamaa kutokana na vizuizi vinavyoweka na FCC, Waziri wa michezo Innocent Bashungwa aingilia kati.

Siku ya leo Bashungwa alikutana na afisa mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez katika kile kinachoaminika ni kujadili kupatikana kwa suluhu baina ya FCC na Simba kuhusu suala la uwekezaji.

Katika mazungumzo hayo Waziri huyo ameeleza kwamba atafanyia kazi suala hilo kwani michezo ni moja kati ya sekta muhimu sana za mapato kwa serikali. Na maendeleo ya timu za Tanzania ndio maendeleo ya Tanzania.

FCC wanadai kwamba mchakato wa mabadiliko wa timu ya simba una mapungufu na inabidi urudiwe hali ya kuwa Mo Dewji anadai wamefikia ukingoni ndipo wanaletewa figisu figisu!

Simba wamekuwa wakifanya vizuri sana na ni wakati sahihi wa mabadiliko hayo kufanyika ili kuisaidia timu hiyo kufanya makubwa zaidi!


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

bashungwa, Bashungwa Aingilia Suala La FCC Na Simba, Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa