Hali ya mustakabali wa Giannis Antetokounmpo ndani ya Milwaukee Bucks imeingia hatua ya mwisho ya maamuzi, huku taarifa zikieleza kuwa uhamisho wa nyota huyo unaweza kukamilika kabla ya NBA Draft ya Juni 23. Baada ya uvumi na mazungumzo ya muda mrefu, inaonekana Bucks sasa wako tayari kusikiliza ofa ili kupata chaguo la juu la draft na kuanza upya.

Kwa muda mrefu, Golden State Warriors walionekana kama moja ya timu zilizokuwa mbele kwenye mbio hizo, lakini sasa wamepoteza nafasi hiyo kutokana na ukubwa wa dau linalohitajika. Hali hiyo imeacha ushindani mkali kati ya Miami Heat na Boston Celtics, huku Heat wakionekana kuwa mbele zaidi katika mazungumzo ya kumsajili MVP huyo wa zamani.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Miami Heat wako tayari kutoa mchanganyiko wa wachezaji kama Tyler Herro, Kel’el Ware, Nikola Jović au Jaime Jaquez Jr., pamoja na chaguo kadhaa za raundi ya kwanza. Hatua hiyo inaonekana kama mpango wa kubadilisha kabisa nguvu za NBA, hasa ukanda wa Mashariki, ambao unaweza kubadilika kwa kasi endapo Antetokounmpo atatua Miami.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Iwapo dili hilo litakamilika, linaweza kuleta athari kubwa pia kwa wachezaji wengine wa ligi, akiwemo Andrew Wiggins. Nyota huyo wa zamani wa Golden State Warriors anatarajiwa kuwa free agent, na kiwango chake cha msimu uliopita akifunga wastani wa pointi 15.4 akiwa na asilimia 41.4 ya mashuti ya mbali, kinamfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaotafutwa zaidi sokoni.

Wakati Miami, Chicago Bulls na Brooklyn Nets wakitajwa kuwa na nafasi nzuri ya kumnasa Wiggins, hatma yake itategemea sana mabadiliko yatakayotokea baada ya dili la Antetokounmpo.



