Kama ambavyo LA Lakers walivyoshindwa kutetea ubingwa wa NBA msimu ulioisha, Milwaukee Bucks wamevuliwa rasmi ubingwa msimu huu.
Bucks walitwaa ubingwa wa NBA msimu ulioipita na wameendelea kufanya vizuri msimu huu ambao walikuwa wanautetea ubingwa wao. Mbio za sakafuni huishia ukingoni, Boston Celtics yawavua ubingwa rasmi.
Ni kwenye mchezo wa 7 kunako fainali ya Eastern Conference alfajiri ya kuamkia leo. Celtics wamewashushia kipigo kikali Milwaukee kwa kuwafunga kwa pointi 109-81 na kuwatupa nje ya safari ya ubingwa msimu huu.
Licha ya Giannis Antentokounmpo kutupia pointi 23, hazikutosha kufua dafu mbele ya Jason Tatum na nyota wenzake wa Celtics ambao walipindua meza kwenye ungwe ya pili baada ya Bucks kuongoza kwa pointi 26-20 kwenye ungwe ya kwanza.
Kwa matokeo haya, Celtics watachuana na Miami Heats kwenye fainali ya NBA Eastern Conference.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.