Baada ya miaka 12, Boston Celtics wamefanikiwa kutinga fainali ya NBA baada ya kuwamwaga Miami Heats.
Licha ya kupoteza michezo 2 ya mwanzo, Celtics walirejea mchezoni na kuipambania tiketi ya kucheza fainali ya NBA 2022. Mpaka wanaingia kwenye mchezo wa 7, matokeo yalikua ni 3-3 baada ya michezo 6.
Jimmy Butler hakuamini kilichotokea baada ya kukosa kupachika mpira wa pointi 3 na kutoa nafasi ya kipekee kwa Boston kutumia mwanya huo kupachika mipira miwili ya pointi 2 na kumaliza mchezo kibingwa.
MVP wa mchezo huu, Jayson Tatum alikua kinara wa Boston kwa kupachika pointi 26 na kutoa pasi 6 za magoli kwenye ushindi unaipeleka timu yake kwenye fainali, uso kwa uso na Golden State Warriors.
Mchezo wa kwanza wa fainali ya NBA utachezwa Alhamisi hii kule San Fransisco, Marekani.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!