Mchezo wa Finalissima uliokuwa uwakutanishe mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Spain na mabingwa wa Amerika Kusini timu ya taifa ya Argentina umefutwa rasmi kutokana na hali ya mvutano wa kisiasa Mashariki ya Kati. Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA lilitangaza Jumapili kuwa mchezo huo uliopangwa kufanyika nchini Qatar hauwezi tena kuchezwa kwa sababu za kiusalama.
Mvutano huo unahusishwa na mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ambayo yameathiri nchi kadhaa za Ghuba. Hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa katika safari za ndege katika vituo vikubwa vya usafiri na kupelekea matukio kadhaa ya michezo kufutwa kutokana na hofu ya usalama.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Machi 27 katika Uwanja wa Lusail mjini Doha. Mashabiki walitarajia kushuhudia nyota wa Argentina Lionel Messi akichuana na chipukizi wa Hispania Lamine Yamal katika pambano hilo kubwa la kimataifa.
Katika taarifa yake, UEFA ilisema kuwa baada ya majadiliano na waandaaji nchini Qatar walilazimika kusitisha mpango huo.
“Ni jambo la kusikitisha sana kwa UEFA na waandaaji kwamba mazingira na muda vimewazuia timu hizi kupata nafasi ya kugombea taji hili muhimu nchini Qatar,” ilisema sehemu ya taarifa ya UEFA.
UEFA ilisema walijaribu kutafuta njia mbadala za kuchezwa kwa mchezo huo, ikiwemo kuupangia kufanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa kugawa mashabiki wa pande zote kwa usawa, au kuchezwa kwa mfumo wa mikondo miwili kati ya Madrid na Buenos Aires. Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Argentina lilikataa mapendekezo hayo.
Kwa upande wake, Shirikisho la Soka la Hispania Royal Spanish Football Federation lilisema lilikuwa tayari kufanya kila jitihada kuhakikisha mchezo huo unafanyika.
“Tangu mwanzo kabisa shirikisho limeonyesha dhamira yake kamili kuhakikisha mchezo huu unafanyika kwa sababu unaongeza heshima na hadhi ya kimataifa hasa katika mwaka wa Kombe la Dunia,” ilisema sehemu ya taarifa ya shirikisho hilo.

