Ronaldo na Messi Walivyotufanya Tushiriki Dhuluma

Frank Ribery amehusika katika kamba 40 msimu mzima, ametwaa tuzo ya mchezaji bora Bundesliga, amebeba treble pale Ujerumani, kabatini amezifungia medali za UEFA, taji la ligi kuu na DFB POKAL akiwa na Bayern Munich, isitoshe amekuwa mchezaji bora Ulaya.

Ronaldo na Messi Walivyotufanya Tushiriki Dhuluma
.
Kule Hispania Ronaldo alikuwa mfungaji bora, alipiga mabao 66 katika mechi zote, Hakutwaa taji lolote zaidi ya kufika fainali ya Copa del Rey. Swahiba wake Lionel Messi alibeba La Liga akirejea kambani mara 42. Hiyo ni 2013.
.
Macho yote yakiwa Paris usiku wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia inatolewa, kila mtu anasubiri Frank Ribery apewe tuzo yake. Maskini ya Mungu hawakujua mfaransa wa watu anaenda kudhulumiwa kama kawaida. Ronaldo aliitwa kama namba moja, Messi namba mbili na yeye akawa namba tatu.

Ronaldo na Messi Walivyotufanya Tushiriki Dhuluma
.
Dhuluma tu, walitaka Ribery afanye nini cha ziada? Alibeba kila taji aliloshiriki mwaka huo. Alikuwa mchezaji muhimu zaidi Bayern Munich. Treble aliyotwaa hata Franz Beckenbauer na Gerd Muller hawakuisogelea. Yeye angefanya nini zaidi? Dhuluma tu na dunia haikujalisha. Kwani Ribery ni nani?
.
Watesi wa Ronaldo wangeweza kumtetea Ribery, ila wangezungumza nini wakati wanajua walichokifanya 2010? Wakafanya walichojua, wakampa Lionel Messi tuzo ya mtu. Dhuluma hii.

Ronaldo na Messi Walivyotufanya Tushiriki Dhuluma
.
Wesley Sneijder akiwa bingwa wa Ulaya, bingwa wa Serie A na mshindi wa Coppa Italia, akaondoka na Scudetto. Akaenda kuifikisha Uholanzi fainali ya kombe la dunia. Usiku wa tuzo Lionel Messi akawa mchezaji bora wa dunia kisa La liga aliyotwaa.

Ronaldo na Messi Walivyotufanya Tushiriki Dhuluma
.
Huyu Sneidjer hakuwa hata tatu bora. Lionel Messi akawa mshindi kwa kigezo cha mabao 47 ya La liga. Iniesta akaja nyuma yake kisha pacha wake Xavi Hernandez katika nafasi ya tatu. Ndiyo hivyo. Golden, silver na Bronze medals zote zikamwagwa Barcelona. Sneijder wa watu akachinjiwa baharini.Hii dhuluma nani atatusaidia?

Ronaldo na Messi Walivyotufanya Tushiriki Dhuluma
.
Tunakubali mlituletea chakula ambacho hatukuwahi kukionja kabla ila hatukujua kama mnatulisha hadi saza mlizowaibia maskini. Siwataji kwa majina. Msipolipwa na Wanadamu mtalipwa hata na historia.


Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

27 Komentara

    mh ayo maneno ya kuzusha ata siyaamini nikiwa kama shabiki

    Jibu

    Hayo ndio maneo yasiyo takiwa kuongerewa maneno yasio yauwakika namaneno yakumpa mtu sifambaya

    Jibu

    Zuluma sio nzuri

    Jibu

    Hakuna ukweli wowote

    Jibu

    Duh sio poa

    Jibu

    Swala la mchezaji bora uwa linahusishwa na mambo mengi sana ambayo ndo uzingatiwa

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Ni vizazi Bora vilivyotokeah kwny soka hv sasa

    Jibu

    Sio poa kabisa

    Jibu

    Mambo haya huwa yanatokea sana

    Jibu

    Duu dhuluma mbaya

    Jibu

    Dhuruma sio nzuri kabisa

    Jibu

    Duuh sio pow

    Jibu

    Sio poa

    Jibu

    Duuh mbona mamb hay awaendan nayo

    Jibu

    Hiyo cauple naielewa sana

    Jibu

    mmh

    Jibu

    Good new

    Jibu

    Makubwa haya

    Jibu

    Vizazi bora vilivyotokeah kwny ulimwenguni wa kabumbu

    Jibu

    Majanga hayo

    Jibu

    Dhuuuu

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Ronaldo na mess ni wachezaj ambao hawatawah kutokea ulimwenguni

    Jibu

    Siyo poa

    Jibu

    Duh

    Jibu

    Habari poa sana

    Jibu

Acha ujumbe