Taifa Stars 0 - 1 The Swallows

Timu ya Taifa Stars ya Tanzania leo imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo wa leo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kipindi cha kwanza timu zote mbili zilitoshana nguvu baada ya kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana.

Kipindi cha pili mambo yalizidi kuwa magumu kwa timu zote mbili ambapo Stars ilijaribu kufanya mashambulizi yalishindwa kuzaa matunda na Burundi ilikuwa ya kwanza kupiga shuti la kwanza ambalo lililenga lango kipindi cha pili.

Bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 84 kupitia kwa Said Ntibazonkiza na kuwafanya Burundi kuibuka na ushindi ugenini.

Simon Msuva nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa haikuwa bahati kwao kwa kuwa walipambana ili kupata ushindi ila mambo yalikuwa magumu kwao.

Stars ilimaliza dakika 90 ikiwa pungufu baada ya kiungo mkabaji Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 78 kwa kuwa alikuwa alionyeshwa kadi mbili za njano.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

31 Komentara

    taifa stars walionesha juhudi za hali ya juu ila bahati haikuwa kwao

    Jibu

    Ni kujipanga upya kipindi kijacho

    Jibu

    Taifa stars wametuangusha watanzania kwa kweli hatukutegemea matokea yale

    Jibu

    Jipangeni upya bahat haikuwa upande wetu!

    Jibu

    Waongeze juhudi na mazoezi yakutosha ili msimu ujao wafanye vizuri

    Jibu

    Taifa stars wanajua kucheza mpira tena vizuri tu ingawa mkude simba alituangusha alivyo pewa kadi nyekundo hapo tulicheza pungufu na kuonyesha uwezo wetu japo tulifungwa ila mpira ulikowa bomba

    Jibu

    Timu yataifa Stars ilionesha ushilikiano kwakweli walijitaidi mpaka izo dakika zilizo salia kupigwa goli moja dakika za majerui walionesha ushindani kwakweli ilandio ivyo matoke kupigwa 1-0

    Jibu

    Tanzania tulistahili kufungwa.

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    Taifa stars sijajua walikwama wapi maana juhudi zao tuliziona

    Jibu

    Sifa ya Wa tz tunajuwa kuongea kuliko vitendo kwenye upande Wa michezo tuna safari ndefu

    Jibu

    Kuteleza sio kuanguka bado wana nafasi ya kujipanga upya!!!

    Jibu

    Mechi ilikuwa nzuri wachezaji walijitahidi kucheza kwa hali ya juu

    Jibu

    Asiye kubali kushindwa sio mshindani na ndio hali iliyotukuta taifa stars ila juhudi tulizionyesha bahat tu haikua kwetu

    Jibu

    Inatakiwa kujipanga taifa stars kwa mechi zingine hiyo inabidi wakubaliane na matokeo

    Jibu

    Taifa stars wamezingua

    Jibu

    Stars wamechez vizur Ila umaliziaj ni mbaya

    Jibu

    Tumetia aibu jamani kufungiwa nyumbani

    Jibu

    Sasa wajiange upyaa

    Jibu

    Daa! Asante kwa taarifa

    Jibu

    Timu yetu ya Taifa inatakiwa ijipange zaidi, sio mwanzo mbaya

    Jibu

    Stars bado sana kisoka inabid timu ikae muda mrefu waelewane

    Jibu

    Timu inatakiwa ikae pamoja kwa muda ili wachezaji wafamiane

    Jibu

    Taifa stars wameniangushaa

    Jibu

    Wafanye mazoezi ya kutosha

    Jibu

    Taifa star wapo vinzur ni bahati mbaya

    Jibu

    Taifa star wanahitaji mazoezi mazito

    Jibu

    Mazoezi Yana hitajika mazito

    Jibu

    TZ tunakwama wapiii

    Jibu

    Taifa stars wametuangusha

    Jibu

    Sawa

    Jibu

Acha ujumbe