Tuchel Chukua Fimbo Nikwambie Wakumchapa PSG

Nadhani PSG wamejifunza siku nyingine, usipotumia nafasi zako basi uwe tayari kupoteza. Walikuwa timu bora uwanjani kwa dakika 60. Walikaba vema, walitengeneza nafasi ila hawakujua namna ya kuuweka mpira kambani. Wangeweza kuongoza mabao mawili kabla Bayern Munich hawajapata bao.

Njia waliyotumia PSG kumdhibiti Sergie Gnabry, ni njia hiyohiyo waliyoitumia Bayern Munich kumdhibiti Kylian Mbappe. Hakikisha yupo mtu karibu kabla hawajapata mpira. Sikushangaa kutokuwaona Joshua Kimich na Juan Bernat wakipanda.

Coman alizikuta akili zake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo walipoenda mapumziko. Kwa kile kipindi cha kwanza alikuwa machachari badala ya kuwa hatari. Pengine hakutegemea kuwepo kwenye karatasi ya majina ya wanaoanza. Aliporejea kipindi cha pili, akaelewa maeneo ya kusimama ili aisadie timu kushambulia zaidi. Kwa dakika 25 za kwanza za kipindi cha pili, alikuwa mchezaji hatari zaidi uwanjani.

Neymar anazidi kutufanya tuamini kuwa Ronaldo na Messi hawatokei ndani ya hii dunia. Siku ambayo alitakiwa asimame kama mchezaji mkubwa kuitetea PSG, yeye alipotea kabisa. Hakuhusika sehemu kubwa ya mchezo. Ni kama alikuwa na mchezo wake peke yake. Kitu pekee alichowasaidia PSG leo, ni kulia baada ya mechi.

Acha tumalize tu na Thiago Alcantara. Yule mhispaniola anajua bwana. Ni kama anaona mara tatu zaidi ya binadamu wa kawaida. Njia anazopitisha pasi, namna anavoendesha timu, misuli yake wakati anakaba. Absolutely heavenly! Alcantara mtu mmoja na nusu.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

34 Komentara

    Rio Ferdinand aliwaambia Man U baada ya kutolewa na Sevilla kwamba unaposhindwa kutumia nafasi unazopata tarajia kuadhibiwa na ndicho walichokutana nacho PSG#meridianbettz

    Jibu

    PSG walikua wanafanya vizuri kipindi cha kwanza …wamekuja kaharibu mwishoo kabsa ..kwr mpira dk90

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Kwa atua waliofika ya fainali wamehitaidi sana

    Jibu

    Psg ni kama washambuliaj wao hawakuwa na umakini wakifik golini kwa bayern chansi za wazi walizopata zilikuwa zinamaliza matokeo mapema

    Jibu

    Watu wengi jana tulikuwa na Imani juu ya PSG kutwaa ubingwa pia walianza vizuri kipindi cha kwanza lakini umakini tuu ndio uliwagharimu PSG na kupokea kipigo cha goli moja lakini pongezi nyingi ziende kwa Kipa Neuer kwa kusave mipira ya hatari kutoka kwa Neymar na Mbapper jana

    Jibu

    kipigo cha goli moja lakin pongezi nging ziende kwa kipa neuer kwa kusevu mipira mingi ya hatari kutoka kwa neymar na mbappe jana#meridianbettz

    Jibu

    Mwenendo wa PSG ulikuwa mzuri Ila ndio mpila kwaio wamejitaidi Sana goli moja sio mbaya Ila PSG walikaza Sana mpaka kufungwa goli moja wamefanya kaz kwampi ule walio kuwa Wana ucheza PSG ulikuwa mzuri nibati mbaya tuu

    Jibu

    psg bahati haikua ila walijitahidi sana kucheza mpira

    Jibu

    PSG mpira waliupa sana ushirikiano ila tu mpira ndo haujawapa ushirikiano wajipange kwa msimu ujao tu

    Jibu

    Sema psg walijitahidi

    Jibu

    Psg ni Kama hawakuwa makini kwa mechi ya jana bahati haikuwa kwao

    Jibu

    Gemu hii ilikuwa ya ushindan mkubwa sana kiukwel kwa pande zote mbili

    Jibu

    Psg walijitahidi sana sema bahati haikua ya kwao

    Jibu

    Mechi ya Jana ilikuwa ina raha yake

    Jibu

    Alkantara ni noma sana.

    Jibu

    Walichezah vzr walitengenezah nafas nyng sema hawakuwah na bahati katika mchezo ule congrat Bayern championπŸ†πŸ†πŸ†πŸ†

    Jibu

    Gemu ilkua ngumu kwa wote ila ndo lazima mshnd apatkane

    Jibu

    PSG wamepambana ila bahat haipo kwao!!!

    Jibu

    Psg haikuwa bahat yao

    Jibu

    Mechi ya Jana ilikuwa ngumu Sana kwa psg

    Jibu

    Siku zote mpira ni mchezo wa makosa unapofanya makosa ndipo mwenzako anatumia makosa yako kukuadhibu PSG wajipange kwa msimu ujao.

    Jibu

    PSG wajipange kwa msimu ujao

    Jibu

    Siku zote waenga wanasema mkamia maji hanywi..!kwa kuangalia pale PSG mbappe alikua na shauku sana ya ubingwa lakini mwisho wa siku hatukuona mbwe mbwe zake kakutana na wanaume wamemana ukutani big sana Bayern

    Jibu

    PSG Jana wametaga Bhana wamezingua sana

    Jibu

    Nilishangazwa sana jana na how marko verrati fundi hakuwepo etii

    Jibu

    Watu wengi jana tulikuwa na Imani juu ya PSG kutwaa ubingwa pia walianza vizuri kipindi cha kwanza lakini umakini tuu ndio uliwagharimu PSG na kupokea kipigo cha goli moja lakini pongezi nyingi ziende kwa Kipa Neuer kwa kusave mipira ya hatari kutoka kwa Neymar na Mbapper jana

    Jibu

    Wamezigu sana pSG

    Jibu

    Psg bahati haikuwa yao ndio maana wamepoteza gemu

    Jibu

    Hapo walipofikia wamejitahidi sana

    Jibu

    Poleni Sana P.SG haikua riziki

    Jibu

    Pole sana kwa PSG

    Jibu

    Psg bahat haikuwa kwao lakini walicheza Sana mpira

    Jibu

    Mpira ulichezwa Lakin Lazima apatikane Mshindi tu

    Jibu

Acha ujumbe