Ni dakika ya 15 tu ya mchezo, Lionel Messi wa miaka 17 anakimbia kutoka chini kwenye counter, anapita katikati ya kiwanja hadi ndani ya box la Real Madrid, anauacha mpira miguuni kwa Eto’o anayezunguka nyuzi 180 na kumtungua Iker Casilas akiwa katikati ya wachezaji wanne wa Real Madrid.

Ronaldinho, Usiku wa Heshima kwa Ronaldinho Pale Santiago Bernabéu, MeridianbetSamuel Eto’o anageuka na kukimbilia majukwaa ya kusini karibu kabisa na alipoketi rais wa Real Madrid Fiorentino Perez. Anamtazama huku akimuonesha nembo ya Barca iliyo kifuani mwake. Dunia ina tafsiri kuwa anamuambia “Mlikosea sana kuniruhusu niondoke”.
.
Bao la Eto’o linaondoka na vichwa vyote vya habari kipindi cha kwanza. Hii ilikuwa dhidi ya Real Madrid iliyosheheni Galacticos. Golini yupo Iker Casilas, kikosini yupo Roberto Carlos katika ubora wake, David Beckham wa Uingereza, Zinedine Zidane na jezi namba tano mgongoni, Raul Gonzalez yule bora kabisa na Ronaldo Nazario wa Brazil.

Ronaldinho, Usiku wa Heshima kwa Ronaldinho Pale Santiago Bernabéu, Meridianbet
.
Baada ya kupoa kwa muda mrefu wa kipindi cha kwanza, Ronaldinho alipokea pasi ya Deco akiwa kushoto kabisa mwa uwanja, akavuka mstari wa katikati kwa kasi ya ajabu, akampiga chenga Sergio Ramos na kumuacha akigaagaa chini bila msaada, kisha akamtambuka Ivan Helguera na kumtungua Iker Casilas ambaye hakujishughulisha hata kuruka.
.
Dakika ya 78 tena, Xavi alipora mpira kwa Julian Baptista, akausukuma kwa Deco, Deco akamzunguka Pablo Garcia ndani ya duara la katikati kisha akauweka tena kwa Gaucho. Gaucho akamtambuka Sergio Ramos na kuondoka kwa kasi ya duma kisha akamtungua Iker Casilas aliyebaki akitingisha kichwa, haamini yanayotokea.

Ronaldinho, Usiku wa Heshima kwa Ronaldinho Pale Santiago Bernabéu, Meridianbet
.
Ndipo hapo mashabiki wa Real Madrid walisimama na kumpigia makofi Ronaldinho Gaucho. Hawakuamini alichokuwa anawafanyia mbele ya macho yao katika uwanja wa nyumbani.
.
Hilo lilitokea siku kama ya leo miaka 15 iliyopita. (November 19 2005)


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

 

16 MAONI

  1. Hakika gaucho ronaldinho alikuwah kwny ubora wa Hali ya juuu katika usiku ule gaucho ronaldinho alikuwah high tempo ya mchezo aliupigah mwingi sana uck ule katika dimba la nou camp hakika hakuna mchezAj yoyote aliyeweza kufikiah kiwango kile alicho kionyesha gaucho ronaldinho imebaki Kama history kwAke na hata club kwa ujumla vile vile na hata kwa mashabiki wake hakika hatuweza kusahau cku hle ronaldinho gaucho mwamba toka brazil rio gienero hakika history iliandikwa uck ule

  2. Hakika historian iliandikwa uck ule legend Ronald inho gaucho alikuwah kwny gud perfume uck ule hakika gaucho hata sahau uck ule nahata mashabik waliozuliah mchezo ule walipata burudani ya Hali ya juu toka kwa gaucho hakika history iliandikwa uck ule

  3. Ronaldinho ndio alikua mfalme wa soka enzi zile hadi leo hajatokea mbdala yake na historia yake ya soka haiwezi kusahaulika maishani

  4. Ronaldo anaistoria nzuri kwenye game lake alilo lipiga nyuma uko kwaio Ronaldo lazima ajivunie kwamengi aliyo yafanya

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa