Klabu ya Crystal Palace imeandika historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA Conference League kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano katika mchezo wa fainali uliochezwa Jumatano usiku. Bao la mshambuliaji Jean-Philippe Mateta kipindi cha pili lilitosha kuipa Palace taji lao la kwanza la Ulaya na kuongeza mafanikio makubwa katika kipindi cha hivi karibuni.
Kocha wa Palace, Oliver Glasner, alisema ushindi huo ni matokeo ya uvumilivu mkubwa wa wachezaji na mashabiki baada ya changamoto walizokutana nazo msimu huu. Palace ilikosa nafasi ya kushiriki Europa League baada ya UEFA kuiondoa kutokana na sheria za umiliki wa vilabu vingi, lakini waliweza kurejea kwa nguvu na kutwaa Conference League.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Wachezaji, klabu na mashabiki wamepata kile walichostahili. Wakati mwingine unapitia njia ngumu kabla ya kufika unapotaka kwenda,” alisema Glasner baada ya mchezo huo.
Glasner, ambaye alitangaza Januari kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu, ameondoka akiwa ameandika historia kubwa ndani ya Palace. Tangu kuwasili kwake mwaka 2024, klabu hiyo ambayo haikuwa imewahi kushinda taji kubwa hapo awali sasa imefanikiwa kunyakuwa FA Cup, Community Shield pamoja na taji la kwanza la Ulaya.
“Mashabiki wanapotushukuru kwa kuwapa siku bora ya maisha yao, nami pia nawapongeza wachezaji kwa kunipa nyakati kubwa ambazo sitazisahau,” aliongeza Glasner.
Beki wa Palace, Tyrick Mitchell, alisema ushindi huo ulikuwa wa kihisia mkubwa baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu huku akieleza kuwa msimu huu ulikuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya michezo waliyoicheza katika mashindano mbalimbali barani Ulaya na England.
Kwa upande wake, kiungo Adam Wharton alisema mashabiki wa kusini mwa London walikuwa sehemu muhimu ya ushindi huo huku akisisitiza kuwa ni vigumu kuelezea furaha waliyoipata baada ya kutwaa taji hilo la kihistoria.


